



![]()




na kufafanuliwa katika usemi wa siku hizi
Gabriele

First Edition in Swahili : October 2021
1ère édition en Swahili : Octobre 2021
Translated from the original German title : Traduit de l'allemand, titre original : Die Zehn Gebote Gottes durch Mose, ausgelegt mit den Worten der Jetztzeit
The German edition is the work of reference for all questions regarding the meaning of the contents Pour toute question se rapportant au sens, l'édition allemande fait référence
© All Rights Reserved/ Tous droits réservés Gabriele -Verlag Das Wort GmbH
Order No. / N° de comm. : B33 8s w • ISBN : 978 -3- 9 6 4 4 6 -480-4 (pdf)
Amri kumi za Mungu, zilizofafanuliwa katika usemi wa siku hizi
Dibaji
«Andiko lina nguvu ya utendaji mara tu mtu anapoanza kuzishika Amri. Ni kwa namna hiyo ndiyo hatua kwa hatua anakomaa katika sheria ya ulimwenguni pote ya upendo na ya Uzima. Ni yule tu anayetekeleza Amri kwa upendo wa dhati na kwa moyo wote ndiye anayo dhamiri ya sheria ya ulimwenguni pote na ni yeye ndiye atakayegundua pia ukweli ulio ndani ya nafsi ya mtu.»
Mungu aliwatolea watu Amri kumi kupitia Musa. Roho wa Mungu ni uhuru. Roho huru, aliye popote, wa milele, aitwaye MUNGU katika nchi za magharibi, ni uzima ulio popote, maisha ilyo popote. Yeye ni nguvu ya ulimwengu, Mto ndani ya jua na sayari tukufu. Ni uzima ndani na juu ya uso wote wa dunia, ni uzima ndani ya kila mmea, ndani ya kila mnyama, ndani ya kila jiwe na vilevile ndani ya kila mtu na nafsi zote. Roho huru, aliye popote, Mungu, ni nguvu iliyo pote ulimwenguni ndani ya kile kisicho na mwisho au mpaka.
Mungu, Wamilele, aliwatolea wanae wanadamu
Amri Zake kutokana na upendo Wake na ambazo ni mashauri halisi ya uzima, sehemu za sheria ya milele na ya ulimwenguni pote ya Yule asiye na mwisho. Jinsi ndani ya mfumo wa Maisha ya milele , wa Uzima wa milele, vyote vimo ndani mwa vyote, hivyo pia kila mojawapo ya Amri imo ndani ya nyingine zote.
Tuna wajibu wa kutimiza Amri za Mmoja wa ulimwenguni pote maishani mwetu duniani, yaani wajibu wa kuzishika badala ya kuridhika na kuzijua au kuzisoma tu. Amri za mungu hazina katazo hata moja. Kwa kuwa Roho huru ni uhuru, hayo yana maana kwamba mwanadamu ana uhuru kabisa wa kukubali maonyo ya Mungu na kuyashika au la.
Kuona kwamba Mungu haingilii kati maisha ya mwanadamu, mtu ni mhusika wa maisha yake, yaani mhusika wa hisi, hisia, mawazo, maneno, na matendo yake mwenyewe. Amri za mungu ni vipengele, au sehemu za sheria ya milele ya ufalme wa Mungu. Amri Zinasaidia wote wanaoitegemea sheria hiyo kuishika na kuitimiza, na kufikia hivyo maadili na wema wa kiwango cha juu, vinavyomtakasa mwanadamu, vinavyotakasa fikra, maneno na matendo yake. Yule anayetimiza
Amri za Mungu hutakasa pia hisia zake na
kuendeleza mitazamo safi ya maisha. Anatambua kwamba mazingira na wanyama ni sehemu pia ya umoja katika Mungu. Kushika Amri za Mungu kunamfanya mtu awe huru na tajiri kiroho.
Amri za Mungu ni pendekezo ambayo Mungu, Roho huru, anamtolea kila mmoja wetu. Anatuomba tuzitekeleze maishani mwetu, kiasi kwamba maadili tunayojifunza hivyo ituwezeshe kuelewa ni nini haki, umoja na upendo wa Mungu na wa jirani. Kwa kutimiza moja kwa moja Amri hizo, tunakaribia uzima ambao ni Roho huru: Mungu, Roho wa ulimwenguni pote aliye ndani ya vitu vyote.
Muda wa utekelezaji huo wa hatua kwa hatua wa Amri, tunakuza mtazamo wa kina sana wa mambo na kutambua pia ndani mwetu wenyewe kwamba Roho huru, aliye pote, yumo pia ndani mwetu.
Tunarudilia: Uzima ni Mungu, Roho huru, aliye Yuleyule ndani ya utamaduni wa kila jamii ya dunia nzima. Ndani ya kila utamaduni, Mungu ni tofauti pia wingi usio na mwisho wa uzima safi. Kila Amri ya Mungu ni mlango unaoongoza kwenye utimilifu wa Uzima, kwani Mungu, Roho huru ni Uzima. Ikiwa kwa namna yetu nzuri ya kufikiri na kutenda, tunazama ndani ya Uzima,
ndani ya vyanzo vya maisha halisi, tunagundua kwamba kila Amri ina sura nyingi za uzima halisi ndani mwake na kwamba kama chanzo cha nguvu, imo ndani ya Amri zingine. Wakati tunaposimulia kuhusu «Roho huru», ambaye katika nchi za magharibi huitwa Mungu, hatuongei kuhusu Mungu ambaye mapadri na wachungaji wanahubiria watu.
Kama mwanadamu, Yesu wa Nazareti alikuwa Mwana wa Mungu aliyechukua mwili wa kidunia, na kama Kiumbe ndani ya Mungu, Yeye ni Mtawala pamoja na Baba wa Ufalme wa Mungu, Kristo wa Mungu, ambaye, katika Yesu wa Nazareti alituletea wokovu na njia inayotuwezesha kurudi maskani kwa Baba yetu. Wakati alikuwepo duniani, alifundisha watu kwamba Baba wa milele na Yeye ni Mmoja, yana maana kwamba Roho moja na upendo mmoja, ukweli mmoja, ukweli wa milele, sheria ya milele isiyo na mwisho inayomuweka mtu huru. Roho wa Kristo wa Mungu yumo ndani ya Baba na Baba yumo ndani ya Kristo wa Mungu: Roho moja, Uzima mmoja, ukweli mmoja.
Roho wa Kristo wa Mungu, alijifunua kupitia
Gabriele, nabii, chombo chake na tena mjumbe wa
mbingu Kumepita zaidi ya miaka 45 sasa. Kama alivyofaya Kristo wa Mungu wakati wetu huu, Yesu wa Nazareti Naye pia anafundisha kwamba
Kristo wa Mungu, Roho huru, hafungamani na dini yoyote ya nje, kwani kila mtu ni hekalu la Mungu, hayo yana maana kwamba hakuna aliye na haja ya hekalu au kanisa lililojengwa na mikono ya mtu kwa ajili ya kumpata na kumuomba Mungu, akili ya ulimwenguni pote na ya milele.
Leo tena, katika wakati huu mpya, Kristo wa Mungu anaendelea kusema. Mungu, wa milele, habadiliki.
Yeye ni Yule Yule, jana, leo na hata kesho. Ni mamoja pia kwa Amri kumi za Mungu Alizotutolea kupitia Musa. Kristo wa Mungu anayejifunua kwa wakati wetu huu, alisema kuhusu hayo ndani ya moyo wa Gabriele, nabii na mjumbe wake, ambaye, kwa wakati huu mpya, akitumia maneno yake, amefundisha mambo yenye umuhimu wa kipekee, kwa sababu miungu ya kila aina imejitokeza kwa wingi.
Tukisadiki Amri kumi za Mungu na kumsadiki pia Yesu Kristo na mafundisho yake – kwa upekee Mafundisho yake mlimani, iliyo mafundisho ya mbinguni – ikiwa tunajiita wakristo au wakristo wa
awali, au tena tukijisifu kwamba tuko wafuasi wa Yesu wa Nazareti, kwa hiyo tunatoa ahadi muda ule ule ya kutimiza madai yetu.
Ila tungependa kuweka wazi jambo moja: kutimiza yale ambayo wa milele alitutolea ndani ya Amri kumi na yale ambayo Yesu wa Nazareti alitufundisha katika Mafundisho mlimani hayana uhusiano hata kidogo na kanuni, masharti na amri za mashirika ya kieklezia.
Amri ya kwanza ya Mungu
«Mimi ni Bwana Mungu wako, usiwe na miungu mingine kando yangu»
Mungu wa Abrahamu, wa Isaka na wa Yakobo, Mungu aliyesimulia kupitia Musa na manabii wakubwa wote wa Mungu, ni Roho huru, sheria ya milele ya upendo wa Mungu na wa jirani.
Mungu, Roho huru, ni nguvu za uumbaji ndani ya vitu vyote. Hata tuende wapi, hata tutazame wapi, ndani ya vitu vyote mna Roho anayetenda kazi milele na milele. Ndani ya kila mwanadamu, ndani mwetu, ndani ya nafsi yetu mna Roho wa ukweli, Roho huru. Anatugusa ndani ya kila seli ya mwili wetu na katika kupumua kwetu. Yote yanayo tuzunguuka, yote yanayoonekana machoni mwetu au la, yana Roho ndani mwake, Mungu, aliye Uzima.
Mwanadamu ana Mungu ndani ya nafsi yake, mwanadamu ni wa kimungu, ila yeye si Mungu. Kiumbe cha kimungu huishi milele kwa sababu Mungu Babaye wa mbinguni alikitazama na kukiumba. Kiumbe safi cha kiungu kinaitwa pia kiumbe cha kiroho.
Neno la Mungu, Amri iliyotolewa kupitia Musa, hutufundisha: «Usiwe na miungu mingine kando yangu.» Yanasimulia kuhusu nini hakika? Miungu na sanamu hizo za kuabudiwa ni nini na ni miungu na sanamu za kuabudiwa ngapi ambayo wanadamu waliumba wakati wa sasa, na ambayo wanatii na kuabudu? Je! ni fedha, kukimbilia teknolojia ya kisasa, kuwa watumwa wa burudani, wa michezo, uchu wa madaraka, tamaa zinazokithiri, kutamani vya wengine na shauku, na vitu vingine vingi tena. Kila tegemeo huhusiana na sanamu yake ya kuabudiwa, inayoabudiwa kwa pamoja na watu wengi katika dunia nzima. Wanadamu huabudia na kutoa sifa kubwa mno kwa wanadamu wengine ambao wanadhani, au wanaowaaminisha, kwa lengo la kuwashikilia, kwamba eti wametumwa na Mungu kuwaongoza au kuwatolea mafundisho. Watu wengi hutoa sadaka kwa miungu, kwa sanamu, hata vilevile kwa wanaojiita waheshimiwa ambao hutukuzwa sana na umma.
Ufalme wa Mungu unaundwa na sifa saba, kama vile pia sheria ya milele na ya ulimwenguni pote, Mungu.
Kupitia Musa, Mungu alitolea dunia yetu itumiayo vipimo vitatu, Amri kumi za Mungu, sehemu za sheria ya milele iliyo na sifa saba.
Kushika Amri za Mungu kunaweza kutusaidia kuelewa uzima wa ulimwenguni pote utokao kwa Mungu. Ni kwa kushika tu Amri hizo hatua kwa hatua ndipo mtu hufikia maadili ya kiwango cha juu. Ni kwa njia hiyo tu ndiyo dhamiri yake husafika, ndiyo anaweza kupata ubainifu na mtazamo wa kina na mpana wa mambo.
Kuona kwamba Mbingu au Ufalme wa Mungu una vipimo saba, si sahihi tujifanyie picha yake, au picha ya mambo yake wala tena kuifananisha na picha ya kile kilicho juu au ndani ya dunia, na angani. Tuyape umuhimu maneno ya Yesu wa Nazareti aliyefundisha kwamba Roho wa Mungu Yumo ndani mwetu, na kwamba sisi ni hekalu la Roho mtakatifu. Picha, sanamu ambazo tunaabudia, kwa mfano sanamu au picha za watakatifu, hujichapa kama picha ya vipimo vitatu ndani ya nafsi yetu. Wakati ambapo mwili ulio ganda la nafsi, huaga dunia, nafsi huenda kwenye makao ya nafsi. Picha hizo za vipimo vitatu, zisizoambatana na Uzima, ambao una vipimo saba, hubaki zikiangikwa kwenye nafsi hiyo. Muda fulani, nafsi itapashwa kutambua kwamba picha hizo ambazo nafsi iliabudu wakati ilikuwa duniani hazina uhusiano na uzima wa milele ambao una vipimo saba.
Kama wanadamu, hatuna uwezo wa kujifanyia
akilini picha halisi ya Ufalme wa Mungu au dunia takatifu za kiroho. Hivyo hivyo si vema kujifanyia picha za viumbe vya kiroho viitwavyo malaika, na hata pia Mungu Baba yetu wa milele, anayeitwa pia Mungu Baba-Mama na ambaye tunamuomba ndani ya sala ya «Baba yetu», hata pia tena Kristo, Mtawala pamoja na Mungu katika Ufalme wa Mungu. Picha na sanamu huhusiana tu na dhana zetu za kiutu. Kwa sababu hizo zote tungepashwa kususia kuabudu sanamu.
Hatungepashwa tena kuabudu mwili wa Yesu uliotundikwa msalabani. Alifufuka tayari katika roho na kama Mwana wa Mungu, Mtawala mwingine wa Ufalme wa Mungu, anaketi kuumeni kwa Baba wa milele. Mwana wa Mungu na Mtawala pamoja na Baba, Yesu, ni Mkombozi wa nafsi zote na watu wote. Yeye ndiye njia, ukweli na uzima, na ni Yeye Kristo anayetuongoza kwa Baba wa milele, katika Ufalme wa milele, ambao una vipimo saba. Msalaba pasipo mwili, kama vile alama ya wokovu unaonyesha njia ielekeayo kwenye Ufalme wa Mungu, Ufalme wa amani, wa umoja na wa uhuru.
Kama vile tumesikia, Roho huru milele ni Uzima ulio popote, ndani ya kila kitu, ndani
ya kila mnyama, ndani ya kila mmea, ndani ya mazingira, ndani ya kila madini na kila jiwe. Uzima unapatikana ndani ya kila tone la maji. Na huo ndio umoja na umoja katika Mungu ni uzima usioweza kufa. Nasi vilevile, wanadamu, ni ganda tu ambamo mna uzima wa milele. Ndani ya nafsi zetu, sisi ni watu wa ufalme wa Mungu. Kama vile mwili wetu ulivyo ganda la Uzima halisi, vile vile pia kila kiumbe cha mazingira duniani, wanyama, mimea, miti, misitu, mawe, navyo tu ni ganda la Uzima. Uzima, nguvu inayoumba inatenda kazi ndani ya kila kitu na ndani ya kila mmoja; ni Roho huru, sheria ya milele, ya upendo wa Mungu na wa jirani. Uzima wa milele na wa ulimwenguni pote unatenda kazi ndani ya vyote vinavyooneka na visivyo onekana. Maada, inayotegemea vipimo vitatu, ni ganda lililo tu picha duni ya uumbaji wa Mungu, na ambamo Uzima ulio na sifa saba unatendea kazi.
Tusimulie sasa kuhusu Amri ya pili, tukimgeukia Roho huru na wa ulimwenguni pote ambaye ni nguvu ya uumbaji.
Amri ya pili ya Mungu
«Usitaje bure jina la Mungu»
Ni vipi tunavyotaja bure Jina la Mungu? Kwa mfano, tunapolitumia jina la Mungu kwa kulaani, kuapa, au tena kwa kusema maneno yasiyofaa, au kwa kusema bure bure: «Mungu wangu, Mungu wangu» bila ya kufikiria kwamba tunataja jina la Mungu pasipo kufikiria juu Yake. Tunatamka neno «Mungu» mara na mara, bila kutambua kwamba tunaongea kuhusu Akili Kamilifu. Tunatamka kila mara, maneno: «Mungu wangu!» au «Asante Mungu!»? Ila tunafikiria nini hakika wakati tunapotamka maneno hayo?
Mara nyingi ni maneno yasiyo na maana, semi za kawaida. Ijapokuwa, kama jinsi tunavyoelewa kwa sasa, yote ni nguvu. Ina maana kwamba ni sisi wahusika wa kila neno linalotoka kinywani mwetu wala si Mungu. Kila mtu alitajaye jina la Mungu bila kufikiria, anataja bure jina la Mungu na hupoteza bure nguvu, na hayo humdhuru yeye mwenyewe.
Kanuni husema kwamba kila tendo husababisha matokeo fulani, kila mmoja wetu ni mhusika peke yake wa mawazo, maneno na matendo yake bali si Mungu Muweza.
Kristo alituagiza kujiswali kila mara: Ninawaza nini? Ninasema nini? Je! Mwenendo wangu unaambatana na masemi yangu, kwa mfano: «Mungu wangu!, Mungu wangu!» au «Asante Mungu!» Yote ni nguvu. Kwa hiyo kuna swali ambalo wanatuswali: Je! ni Mungu ndiye anayetuadhibu wakati tunatenda kinyume cha nguvu yetu wenyewe, ambayo inahusu vilevile maisha yetu duniani? Hapana, tunajiadhibu sisi wenyewe tunapopunguza nguvu yetu ya uzima, uwezo wetu wakutenda.
Maneno haya hutumiwa pia zaidi: «Mungu asifiwe, nimefanikiwa kufanya hiki au kile!», au tena «Mungu asifiwe, hakuna jambo baya lililonipata!» Je! kwa kweli tuna shukurani kwa Mungu? Au si maneno matupu na yasiyo na maana ambayo tunatamka bure, au si semi tu za kawaida? Kwa bahati mbaya, si kawaida kwetu tuyape maana mambo kama na hayo na kuchukua fursa ya kuyafikiria sisi wenyewe, kufikiri juu ya mwenendo wetu, juu ya maisha yetu na pia juu ya yale ambayo tunapanda katika uwanja wa nafsi zetu kupitia fikira na maneno yetu ambayo dhamiri yetu inatambua au la.
Tungepashwa kuwa na dhamiri ya kwamba yale tunayopanda siku moja yatakua na kuzaa
Ni vema kutofautisha maneno «unapashwa» na «tunapashwa».
«Unapashwa» inahusu mtu peke yake, na hutumiwa kwa mtu binafsi, na inaenda kinyume cha uhuru tuliopewa na Mungu.
Lakini, neno «Tunapashwa» ni kwa wote kwa jumla na haihusu mtu binafsi, isifipokuwa tu katika shuruti. Kwa hiyo amri hiyo hugeuka kuwa ya mtu peke yake na kwenda kinyume cha uhuru. Hayo hutokana na Mwenendo wa kutomuacha huru jirani ambao kwa kifupi umo katika kauli: Tenganisha, Funga na Tawala!
17 matunda. Itakuwa je basi? Yule anayeamini kwamba kila tendo husababisha tukio lake, mbegu mavuno yake, na sababu matokeo yake ataelewa kwamba wa Milele anyeitwa Mungu katika nchi za magharibi haadhibu. Kwa hiyo hatushurutishi kwa chochote kile. Amri zake si shuruti ila ni pendekezo ambayo inaweza kuongoza mwenendo wetu. Mwanadamu ana uhuru wa kuwaza, kusema na wa kutenda jinsi apendavyo. Na ni ndiyo sababu tupo wahusika wa matendo yetu na vyote ambavyo tunahisi, tunawaza, tunanena na kutenda siku baada ya siku.
Kupitia Musa, Mungu, wa milele, anapendekeza Amri kutoka sheria yake ya mbingu. Amri kumi za Mungu sambamba na mafundisho ya Yesu wa Nazareti, kabla ya yote mafundisho yake mlimani, vyote pamoja ni njia inayoongoza kwenye Ufalme wa Mungu.
Kristo ndiye Mtawala pamoja na Baba wa ufalme wa Mungu. Vyama vimoja vya kisiasa, hutumia vibaya vilevile navyo jina la Kristo. Jina la Mungu Mtukufu na la Mwanae hayana uhusiano na siasa. Tunaweza kujiswali, kama halitumiwi tu kwa lengo la kudanganya watu? Yeyote anayetaka kuchunguza ukweli wa hotuba za watu wengi, hata katika vyama vya kisiasa vinavyojigamba kuwa vya kikristo, na hata pia mwenendo wake, anaweza kubaini madai hayo kwa kufuata shauri ambalo Yesu alitutolea katika mafundisho yake mlimani, ambayo inasema: «Mtawatambua kwa matunda au matendo yao.»
Yule anayeheshimu Amri Kumi za Mungu na mafundisho ya Yesu wa Nazareti atatambua na kuelewa ni kwa kiwango gani Jina la Aliye juu na la Yesu Kristo linatumiwa vibaya katika vyama vya kisiasa vinavyojiita vya kikristo, na hata katika madhehebu na makanisa inayojiita ya
kikristo. Kila mmoja atajitetea mwenyewe mbele ya sheria ya milele, mbele ya Mungu, kuhusu kile anachojidai kuwa au kuhusu upande gani anaoutegemea. Ni mamoja pia kwa mwanamemba wote anayetambua kwamba kosa limetendeka katika shirika lao na kunyamaa kuhusu jambo hilo.
Makanisa ya kishirika, huzungumzia kuhusu
Mungu anayeadhibu. Kufuatana na kanuni ya uhuru, tunajiadhibu wenyewe wakati tunafahamu
Amri za Mungu na kuzitupilia mbali. Sheria ya milele ni upendo wa Mungu na wa jirani. Ndani ya sheria hiyo mna kipengele cha uhuru pia.
Yule anayetii kanuni ya makanisa inayojiita ya kikristo inayosema: «Unapashwa», pia yule anayeamini hukumu wa milele, adhabu ya milele, hajafikiria bado kwa kweli, jinsi Amri za Mungu na mafundisho ya Yesu wa Nazareti vilivyotumiwa vibaya.
Wa milele, Roho huru, anatuhimiza siku zote kujifunza kuelewa maana ya maneno, hayo yanahusu vilevile Amri za Mungu. Maneno ya binadamu ni ganda tu, hivyo hivyo mwanadamu ni ganda inayoficha uzima wa kweli, mwanadamu ni ganda la nafsi tu. Basi maneno ni maganda, na cha muhimu ni kile kilicho ndani mwao.
Ni Wakati ambapo tunakuwa tayari kupata ukweli ndani ya Amri za Mungu na ndani ya maneno ya Kristo wa Mungu na kuyatimiza maishani mwetu siku zote, ndipo tutapata maarifa ya roho huru, asiyeshurutisha kwa chochote na asiyeadhibu.
Mara nyingi tumesikia wakisimulia kuhusu kanuni ya kupanda na kuvuna, kuhusu kanuni ya sababu na matokeo yake, kwamba kila tendo huwa na matokeo yake.
Methali moja ya kale ya Kijerumani inayotumiwa pia sana bila ya maana yake kueleweka vizuri, husema hivi: «Yeyote asiyetaka kusikia hupatwa na matatizo.» Ni kusema yule asiyetaka kusikia maonyo anayopewa na Mungu, hufuata njia zake mwenyewe. Hawezi kuchukua mtu fulani wala tena Roho huru aitwaye Mungu katika nchi za magharibi kama wahusika wa mawe anayoipanda mwenyewe njiani mwake yaani hali mbovu zilizo ndani ya hisi, mawazo na maneno yake. Mtu anapoteleza muda Fulani kwenye vikwazo alivyoviweka mwenyewe njiani mwake, mara nyingi hutaja Mungu kuwa mhusika. Kwa hiyo methali hiyo «Asiyetaka kusikia hupatwa na matatizo», vilevile pia kanuni inayosema «Mtu huvuna kile alichokipanda», haipewi umuhimu.
Anayefikia kupatwa na yale aliyoyarikodi mwenyewe ndani mwake, matokeo mabaya ya matendo yake, alipashwa kufahamu kwamba hayo ni matokeo ya kutenda kinyume cha Amri za Mungu, na Mafundisho ya Yesu wa Nazareti, na kinyume cha misaada kadhaa iliyotolewa na Roho huru, yaani Mungu. Mashaka na shida, mateso na vinginevyo tena haviambatani na mapenzi ya Mungu, ila ni madhara ya hali ya kufikiri na ya mwenendo wa kipumbavu wa mwanaadamu. Wakati mtu huyo anaposikia kamba zinazomfunga, mara nyingi hajutii ila anamshtaki Mungu: «Kwa nini Mungu anaruhusu haya?» Hangefanya vema kujiswali mwenyewe: «Kwa nini nilisababisha hayo yanipate?»
Tulipashwa kabisa kuwa na dhamiri kwamba sisi ni wahusika wa hisia, fikra, maneno na matendo yetu. Wamoja wanaweza kupinga: «Lakini hayo hayana uhusiano na uhuru. Mungu alipashwa kutusaidia na kuturuzuku, Mungu alipashwa kutulinda!» Wa milele yupo upande wetu na anatuunga mkono. Anatusaidia na kutulinda. Ila ikiwa hatuhitaji jambo hilo, tukikataa mkono wake anaotunyooshea kwa kutokutii Amri zake na mafundisho ya Yesu wa Nazareti, matokeo yake yatafananishwa na hayo yanayofasiriwa
ndani ya mfano tunaowatolea sasa: Baba mmoja alimuambia msichana au mvulana wake: «Fanya angalisho, usifanye jambo hilo, kwa maana, lina madhara yake». Msichana au mvulana akawaza pengine: «Nyakati zimebadilika, anayoyasema baba si muhimu, nitatenda yale nipendayo».
Na ijapokuwa tahadhari ya baba iliyotajwa hapo juu, pengine watoto watafikiri mara tena: «Baba anasimulia kuhusu nini? Ni madhara gani baba anayasimulia?» Na pengine vilevile watakwazika, vilevile na kukasirika na kujibu: «Tupo tayari kukubali madhara hayo!» Namna gani baba atakavyojibu? «Siwezi kuwashikilia kwangu na kuwalazimisha kukubali mashauri yangu. Mpo huru kutenda jinsi mnavyohamuru, walakini kila mmoja anapashwa kukubali matokeo ya matendo yake.»
Ni mamoja pia kwa Mungu, Baba yetu wa mbinguni. Ikiwa watu, pamoja na kufahamu Amri za Mungu zilizotolewa kupitia Musa na Mafundisho ya Yesu wa Nazareti, hawavikubali na kuwaza: «Mashauri hayo hayana nafasi na hatuyajali, nyakati zimebadilika, tunafanya kile tutakacho», Mungu hatawalazimisha kwa chochote na hatawaadhibu, kwani kila mmoja yupo huru. Mungu, wa milele, amepana uhuru
kama urithi kwa viumbe vyote na kwa watu wote. Roho wa milele, Mungu, na Mwanae Yesu Kristo wanapatanisha, wanasamehe na wapo hapo kwa kutuunga mkono mara tu tukitaka na tukimpigia hatua moja Roho huru aliye popote, na tukiheshimu kile alichotuamuru, ni kusema sehemu ya sheria ya milele ya upendo wa Mungu na wa jirani yaani Amri Kumi na Mafundisho ya Yesu wa Nazareti, kwa upekee, Mafundisho yake mlimani.
Tujiswali swali hili :Mungu, wa milele, angetulinda dhidi ya jambo lipi? Je! Atulinde na madhara tuliyosababisha wenyewe kutokana na mwenendo wetu mbovu wa kiburi? Tujiswali tena: Mungu angetenda hivyo, tungeweza kugeuka watu sahihi siku ifuatayo yaani watu waangalifu wanaorekebisha fikra na mwenendo wao, watu wasiorudilia tena siku zijazo maovu iliyowasababishia mafarakano ? Au basi tutaendelea kuchohea maovu hayo?
Amri ya tatu ya Mungu
«Heshimu siku ya Sabato»
Leo, hatuwezi kusema tena kwamba sabato ni siku ya mapumziko kwa watu wote. Kwa sasa, wafanya kazi, wanapashwa kukubali mashuruti ya viwanda ambamo wanafanyia kazi. Isitoshe, sabato ya jumla kwa wote haiwezekani kwa mfano kwa wale wote wanaofanya kazi kwa zamu isiokoma au wanaotumika katika sekta ya malisho.
Sheria ya milele, sheria ya upendo wa Mungu na wa jirani inayotetea pia uhuru haibagui mtu.
Haijalishi siku Fulani ambayo tuna mapumziko jumani, ingelikuwa vema tutumie dakika chache kwa kufikiria juu ya siku zilizopita, kubaini mambo iliyokuwa mazuri na iliyokuwa mabaya hata pia yale yasiyoridhisha jumani. Vyote, hata pia masimulizi yetu vina taarifa ambayo tunaweza kupokea, zaidi wakati hisia zetu .kwa namna nzuri au mbaya, ziliguswa. Muda ambapo tunajihisi vibaya ndani mwetu,msaada ambao tungetumia ni kujiswali wenyewe «kwa nini hivyo». Swali hilo «kwa nini» laweza kutusaidia kuchanganua jambo ambalo pengine tulisahau au ambalo tulitupilia
kwenye sehemu ya chini sana ya ufahamu.
Tunaweza pia kuomba moyoni na kukumbuka kwamba nguvu safi yenye uwezo iitwayo Mungu sehemu za Magharibi, inatenda kazi ndani mwetu na inatamani kutuunga mkono.
Ikiwa fikra zinakusukuma kwenda kuomba kanisani, soma yale ambayo Yesu wa Nazareti alitufundisha. Upande mmoja, alifundisha kwamba kila mtu yeye mwenyewe ni hekalu la Mungu kwa kuwa Mungu hukaa ndani ya nafsi ya mtu.
Upande mwingine, alifundisha yafuatayo kuhusu kuomba: «Lakini wewe, wakati unapoomba, ingia katika chumba chako cha ndani, funga mlango na omba Babako aliye katika siri, na Babako aonaye kwa siri atakujibu.»
Kila mmoja miongoni mwetu ni huru kuomba, kuwaza na kutenda kama apendavyo, wewe kama vile sisi. Ila tusisahau kwamba sisi wenyewe ndio wahusika wa vyote tunavyovitenda na tunavyosahau kuvitenda, sisi ni wahusika wa mwenendo wetu wote.
Amri ya nne ya Mungu
«Tukuza (Heshimu) baba yako na mama yako»
Wakati wa sasa, watu hujipa kila mara utukufu wao wenyewe. Watu pia hutukuza watu wengine.
Hayo ndio hutendewa watu wanaofanya uvumbuzi wa hali ya juu au tena wale ambao, kupitia watu walio na vyeo vya juu serkalini, hupanda daraja ya jamii. Leo wanamichezo mashuhuri katika mashindano, wahigizaji na wasanii na hata watu ambao huonyesha anasa na utajiri wao kwa wote, wao pia husifiwa na kutukuzwa. Inasemeka kwamba watoto wanapashwa kutukuza wazazi. Je! Inatupasa basi kutukuza wanadamu?
Machoni mwa Mungu, sote tupo sawa.Tupo kaka na dada, watoto wa Baba Mmoja aliye
Mbinguni, kama jinsi alivyotufundisha Yesu wa Nazareti. Yesu aliwaambia wale waliokua wakifundisha watu kwa Jina la Mungu wa milele: «Lakini ninyi, msikubali kuitwa Rabi, kwa kuwa mmoja ndiye Bwana wenu, ninyi wote ni ndugu. Na msiite mtu yeyote Baba duniani, kwani mmoja ndiye Baba yenu, Baba wa mbinguni… Mkubwa kati yenu atakuwa mhudumu. Anayejikweza atashushwa na anayejishusha atainuliwa.»
Hata kama mtu ana cheo cha sifa alichotolewa, au sifa anazojipa, mtu asiye na cheo au daraja fulani, machoni mwa Mungu, ni sawa na yule aliyetolewa cheo cha sifa. Hayo ni mamoja pia kwa wazazi wetu. Neno la Mungu ni sheria ya milele, uzima wa kweli. Neno la Mungu linasema tena: «Mchukuliane mizigo», ina maana msaidiane ninyi kwa ninyi.
Ndani ya sheria ya ulimwengu pote na ya mile ya usawa, ya uhuru na ya umoja, hairuhusiwi kwa mtu kujipa mwenyewe sifa na hata pia kuacha wengine wamtukuze. Upendo wa Mungu na wa jirani una ndani mwake pia heshima kwa jirani. Hayo yanamaanisha kwamba ni vema kuheshimiana sisi kwa sisi, na kumtukuza Mungu, Roho akaaye pote ambaye ni Uzima ndani ya kila mtu na vitu vyote, ni vema kuheshimu viumbe vyake ambavyo ni watu, wanyama, mazingira na Ardhi-Mama. Ni yule tu anayeheshimu Uzima ndiye anamtukuza Mungu. Anayeharibu Uzima anadharau Mungu.
Amri ya Tano ya Mungu
«Usiuwe»
Amri ya Tano inahusu mauaji ya aina tofauti. Ila Ngazi za juu za mashirika ya kieklezia, zikabadili neno «kuua» na «kuua mtu kwa kukusudia». Kufuatana na maana ya sasa ya Amri hiyo, inaruhusiwa kwa mfano kuua vitani; ila kuua kwa hiari ni dhambi. Tujadilie ubaya wa «Vita» kwa mujibu wa mafundisho ya Yesu wa Nazareti inayosema: «Wote waushikao upanga wataangamia kwa upanga.»
Yesu wa Nazareti alikua sana mtu wa kupenda amani. Mafundisho yake pia ni ya upatanishi. Yesu alikuwa mtu wa amani na ni Mfalme wa Mbinguni wa amani. Yule aliye badili neno «kuua» likawa «kua mtu kwa kukusudia» na kupunguza maana yake anapenda vita na hakubaliani na Mafundisho ya Yesu wa Nazareti. Machoni mwa Mungu, Baba wa mbinguni ambaye Yesu alitufundisha kumjua, tupo wote ndugu na dada waliopokea uzima, Uzima wa milele toka mikononi mwa Mungu, Baba yao wa milele. Tunapumua kwa kuwa Uzima, ulio nguvu iliyo na uwezo wote ndani mwetu hutiririka ndani ya pumzi yetu. Ni nani aliye na ruhusa na
anayejipatia haki ya kusitisha uzima wa dada au nduguye?
Yesu wa Nazareti alitufundisha kwamba haturuhusiwi kuua mtu. Hayo ni mamoja pia kwa tendo la kuua mnyama kwa hiari na hata kukata mti mbichi. Sisi wanadamu tumeagizwa kutunza ulimwengu na aina zote za viumbe vilivyomo, kuvipenda na kuviheshimu, kwa kuwa ndani ya kitu chochote mna Uzima. Ni Roho huru akaaye pote, ndiye mwenyewe aliye Uzima ndani ya kila mtu na ndani ya kila kitu.
Watu wa sasa kwa kipekee wanajitenga mbali na ukweli wa milele ambao katika nchi za magharibi huitwa Mungu. Kwa bahati mbaya wachache sana hufikiria kwamba Yeye ni Roho Muweza yote Asiye na mwisho, Muumba ambaye nguvu yake ya Uzima hupatikana ndani ya vitu vyote. Malimwengu mbalimbali, sayari, jua tukufu, hata pia mnyama mdogo aishiye duniani, vyote vina Uzima wa Roho wa milele, wa Muumba wa kila kiumbe ndani mwao. Ni nani basi aliye na ruhusa ya kuharibu Uzima ulio wa milele? Uzima ulipewa na nani? Uzima ni wa nani? Mwanadamu, mnyama, viumbe vingine vyote, wote, wana haki ya kuishi hadi mwisho wa maisha yao duniani. Kila mwanadamu, viumbe vyote kwa jumla, vina
haki ya kuishi kama maada ghafi hadi muda wa kurudilia kwao Uzima wa milele, kama viumbe vya kiroho.
Mara nyingi, mtu wa siku hizi hazingatii kanuni ya panda na vuna, inayosema anachopanda mtu ndicho atakachokivuna.
Tukitazama kwa makini dunia yetu inayotawaliwa na majivuno na unyonyaji wa faida za watu na uaribifu wa mazingira kwa ajili ya kujitafutia faida, tutatambua kwamba mbegu mbaya (uovu) haziendelei kufikia upevu lakini zimekwisha komaa, ni kusema madhara yake ni tayari kujitokeza. Lakini ni nani anayeyajali?
Wamoja huyajali, wengine si sana na hufikiri: «Mimi mwenyewe ni mwenzangu. Hayo hayanihusu.» Ijapokuwa hayo, sote tunahusika, sisi kama vile wewe, kwani tuna uzima na uhuru wetu, ambavyo vilisababisha kanuni ya maanguko au upotevu, kanuni ya sababu inayosema: Anachokipanda mtu, ndicho atakachokivuna.
Hakuna aliye na haki ya kuua kwa hiari, hata iwe vitani au mawindoni, au pia kwa sababu anatumia vibaya ardhi au msitu: hakuna aliye na haki ya kuua kwa utashi wake. Anayeua kwa hiari yake yaani kwa makusudi, hupinga kanuni ya Uzima na hata pia Mungu Muumba. Matokeo kwa
kila mtu ni: upandacho ndicho utakachokivuna siku moja, kwa sababu nafsi ya kila mwanadamu huishi milele. Siku moja, baada ya kifo, nafsi itakapokuwa katika makazi ya wafu au ahera, yatastahimili madhara ya matendo, ambayo kama mwanadamu, aliyofanya wakati wa umwilisho wake.
Amri ya sita ya Mungu
«Usizini»
Uzinifu ni aina ya usaliti, ni utovu wa uaminifu. Msingi wa ndoa ni uaminifu wa waliooana. Mke au mume akivunja huo uaminifu kwa kupendelea uhusiano wa kimwili na mtu mwingine, anavunja uaminifu huo wa mtu na mwingine.
Siku hizi, uaminifu ndani ya ndoa ni wa muda kitambo kwani wakati huu vyote hubadilika haraka sana. Watu wanapendelea kujinufaisha na maisha. Leo wanaahidiana uamhinifu, na kesho yote huwa tofauti. Ni mamoja pia popote katika nyanja za ajira. Watu husaini mapatano ya kazi ambamo mna kipengele cha uaminifu. Lakini mara tu itakapohusu faida ya mtu binafsi, na wakati njama na hila vikitumiwa, mkataba huo wa kazi hugeuzwa kuwa hati isiyo na thamani.
Katika nyanja zote,wakati wetu huu wa sasa, watu huongozwa na kanuni ya kupoteza kitu fulani ili kupata faida. Ni kawaida mtu kuachilia familia yake kwa ajili ya uhusiano wa mpito. Hajali mke na wanae wakiwa hatarini au la. Mara nyingi, Wao ndicho kitu cha kupoteza kinachohitajika na wakati huu wa mambo isiyodumu. Uzinifu, kukosa uaminifu, au usaliti,
yote hayo huwa ni kawaida. Mtu hajali mwenziwe, haheshimu tena saini yake iliyo chini ya mkataba wa kazi. Jambo la kupoteza ili kufaidika lina sura nyingi. Maisha katika dunia ya leo yaweza kufananishwa na mchezo wa mche uliochapwa namba moja kila upande, toka moja hadi sita. Siku moja ni namba 1 ndio tunategemea, siku ifuatayo chaguo la moyo wetu au tegemeo letu laweza kuwa namba 3, 5 au 6.
Watu wamoja husema kwamba: «Amri za Mungu zimepitwa na wakati, na kwamba zilitolewa kumepita maelfu ya miaka sasa, na hatimaye amri hizo ni kwa watu wa kale sana!» Hakika, waumini wengi wa wakati huu wa msukosuko wanaukubali leo kwamba ni lazima mtu ajifurahishe maishani kwa hali na kiwango chote kile hata kama hayo inawaathiri na kuwatesa wale waliotelekezwa ambao watakaopatwa na madhara ya anasa hiyo. Ila, hata kama leo tunachukua mienendo potovu nyingi kama ya kawaida bila kuyaonea aibu, Mungu, wa milele,Yeye ni Yuleyule jana, leo na kesho. Sheria yake ya ulimwenguni pote na ya milele ni kamili, ipo na haibadiliki milele na milele. Na wakati Amri ya sita husema «Usizini» yana maana pia «Utatimiza ahadi yako» kuhusu uaminifu wa kweli, imani ya kweli, iwe ndani ya
ndoa au kati ya waliooana kwa jumla na hata pia kazini. Kama vile mtu wa kale, anayeitwa mtu wa shimoni, mtu wa sasa, katika enzi ya teknologia, anayoiita wakati wa kuangaziwa, ana wajibu wa kulinganisha Amri kumi za Mungu na mawazo, maneno, hata pia mwenendo wake wote.
Ndoa, mke na mume na aina yote ya ahadi ilio kama mkataba, ingepashwa kujengwa juu ya ukweli, uwazi, uaminifu, unyofu, na imani. Yule anayezingatia kikamilifu Amri za Mungu na Mafundisho ya Yesu wa Nazareti, Kristo wa Mungu, ambayo ilitolewa miaka 2000 iliyopita na kuyashika hatua kwa hatua, huongeza upeo wa macho yake ya kiroho na huona vitu kwa undani sana.
Kwa mfano anaweza kutambua yule anayemshugulikia na yule ambaye anaweza kumtumainia. Amri ya sita inatuambia «Usizini».
Matengano ni matengano. Kitu kilichokarabatiwa si kizima tena. Ndio maana ni vizuri kujichunguza mwenyewe kabla ya kutenda tendo mbaya, yaani yanayoweza kuleta matengano au kuharibu kitu fulani. Au tena, ni vema mbele ya yote kufikiri kabla ya kuvunja kitu chochote kwa sababu kuunga vipande kunachukua muda, na vipande vyote, hata
viungwe, haviundi tena vizuri kitu cha awali. Matengano mengi husababishwa na kanuni ya panda na vuna inayosema: «Unachopanda ndicho utakachovuna.»
Amri ya saba ya Mungu
«Usiibe»
Tunaweza kubali kwamba tendo «Kuiba» hutaja mitindo nyingi za wizi; wa kwanza ukiwa ni wizi wa vitu. Lakini, kuna mitindo mingine. Kwa haraka tunasema bila ya kufikiria: «Mimi si mwizi!» Lakini tunaweza kuhakikisha hayo kwa urahisi ijapokuwa tunafahamu kwamba yote ni nguvu na kwamba muda, pia nao ni chanzo cha nguvu?
Ni mtu yupi mwizi? Tunaweza kumwita mwizi mtu anayechukua pesa au mali isiyokuwa yake.
Lakini mwizi vilevile ni yeyote anayechukua muda wa mwenziwe, kwa kutumia maneno ya sifa na mabishano marefu yasiyo na maana inayojaa «ndio-lakini» yasiyo na faida au wakati mtu anatumia muda mwingi kwenye mazungumzo ya juujuu. Lakini, mwizi ni mtu yeyote pia anayeomba afanyiwe kitu fulani na mwengine ijapokuwa anaweza kifanya mwenyewe. Au tena yule anayebishana na mwenziwe kwani wote wawili wanajidai kuwa sahihi, na kati yao hakuna anayekubali hata kidogo maneno ya mwengine.
Kupoteza muda yaani pia kupoteza nguvu, kunaonekana katika hali na mitindo mbalimbali
ambayo hatutaweza kutaja yote hapa. Mambo
hayo yote na mengine pia ni namna ya kuiba nguvu za mwenziwe kwa kiwango cha juu sana.
Kila mmoja wetu kwa kweli anao uwezo wa kutaja mifano kadhaa za aina hizo za wizi.
Lengo letu si kutaja aina tofauti za wizi. Cha
muhimu ni kujiswali mwenyewe ni muda upi tunatenda kinyume cha Amri ya Mungu «Usiibe»?
Amri ya nane ya Mungu
«Usishuhudie mwenzio uongo»
Kushuhudia uongo kunamaanisha kusema uongo dhidi ya mtu fulani. Mbele ya mahakama, hayo yana maana kudanganya kuhusu wewe mwenyewe, au kuhusu mtu mwengine. Kumtukuza mtu, kumsifu mno, kumuhimiza katika mwenendo mbaya, na tena kutumia maneno iliyo tofauti na mawazo yetu ni ushuhuda wa uongo ulio kinyume na Amri ya nane.
Kuhakikisha kwamba maoni yetu tu ndio ukweli, nayo yanaweza kuchukuliwa kama aina ya uongo. Kuwa na maoni kuhusu jambo fulani, kutokatana na maana ya neno maoni, yanaonyesha kwamba hatuna uhakika kuhusu jambo, maoni yetu, tunayochukua kama vile ukweli, ni mara nyingi namna yetu binafsi ya kufikiri iliyo sahihi kwetu. Tunasema kwamba ni maoni yetu ila, kufutana na maana, maoni ni dalili ya ukosefu wa ufahamu kamili, kwa hiyo maoni yanaweza kuwa si sahihi na kuwa kama ushuhuda wa uongo.
Kushuhudia uongo kunaweza kuwa pia tendo la kutangaza fununu za uongo kwa lengo fulani.
Fununu zawezesha watu kushtaki wengine. Hayo vilevile yanaenda kinyume na Amri ya nane.
Hatungepashwa basi kufanya ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yetu ila kujiuliza sisi wenyewe mara na mara kwamba fikra na maneno ni yetu hakika, kwa kuwa yote tunayotoa ni nguvu na yataturudilia siku moja au nyingine, hata kama tulisema ukweli au uongo. Yule anayetegemea maadili angelipashwa mwenyewe kujiswali: «je! yale ninayokusudia kusema yanategemea ukweli hakika, au huo si ushuhuda wa uongo ninaoutamka dhidi ya jirani yangu?»
Tukijitahidi kutafakari Amri ya nane, kufikiria ushuhuda wa uongo na pia kufikiria jambo kwamba yote ni nguvu, hata pia fikra zetu, tungelipashwa kutambua kwamba kila mmoja wetu ana wajibu juu ya nguvu anayoitoa, iwe katika fikra, maneno au matendo. Kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunasema ukweli, tungepashwa kabla ya yote kutathmini kile ambacho tunataka kukihakikisha.
Tungelipashwa kuzingatia zaidi kwamba yote ni nguvu na kwamba aina zote za nguvu tunazozitoa, iwe bora au mbovu, zitaturudilia siku moja
au nyingine. Kushuhudia uongo ukifahamu ni kudanganya.
Amri ya tisa ya Mungu
«Usitamani mke wa mwenzio»
Kitenzi «kutamani» kina maana moja na tamaa, nia ya kumiliki, hamu ya kuchukua kitu tunachokitamani kama vile kitu chetu. Neno «Kutamani» ndilo linalotuwezesha kuelewa maana ya utashi wa kumiliki, na wa kujiwekea watu na vitu visivyo vyetu. Mtu akikidhi tamaa yake, ya kumiliki mke wa mwenziwe, kulingana na Amri ya tisa, mke hugeuka milki ya yule aliyempata kwa tamaa. Kwa maana pana kabisa, twaweza kusema hata kwamba mke yule amekuwa mtumwa wa yule aliyemtamani kwa hiari na kwa dhamiri.
Ni mamoja vilevile wakati msingi wa tamaa ni mume, hata pia mtoto ambaye anatamaniwa na kumdhulumiwa kingono. Mume anapotamani mke, au mke anapotamani mume, au tena msingi wa tamaa ukiwa ni mtoto, swali hili: «Ni kwa lengo lipi?» laweza kutusaidia kuelewa.
Tamaa mara nyingi hutegemea kujamiana kimwili na husababisha utegemezi mwingi, aina ya utumwa wa nyakati za sasa.
«Mtumwa», yaani mke, mume, hata pia mtoto aliyetendewa dhulma na aliyetumika vema, muda wote ambapo huwa hana tena faida, hutupiliwa.
Mtu huyo mara na mara hukumbwa na uzuni, na ukosefu wa tumaini, na hisia ya kutumiwa kwa faida ya wengine, kudhulumiwa, na baadaye kutupiliwa. Mtoto aliyetiwa dosari, mara nyingi
hubaki katika hali mbovu sana na huathirika kimwili pia kisaikolojia. Madhara ya mateso hayo ni mara na mara chuki, na nia ya kulipiza kisasi. Kwa yule aliyemtenda hivyo mtoto na kumdhulumu, ingelikuwa heri asingelizaliwa.
Maneno ya Yesu kuhusu jambo hilo ni wazi: «... yeyote atakaye potosha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutupwa katika kilindi cha bahari.»
Neno «tamaa» lina sura tofauti kama vile, kupevusha mtumishi wa taaluma kubwa wa kiwanda fulani toka kazi yake kwa ajili ya kujipatia faida kupitia ufahamu wake au tena kupeleleza siri za kiwanda, yote hayo yakilenga pesa na sifa. Kwa maana pana, yanaweza chukuliwa kama vile biashara ya watumwa. Mfano huu ni mojawapo ya mingine. Tamaa ina sura nyingi. Jambo moja ni kweli: anayepokea hongo na kunaswa ndani ya mtego wa tamaa ya mwenziwe hugeuka mtumwa wa nyakati za sasa aliyejitoa kwa mnunuzi wake. Anapoteza hivyo uhuru wake, hadi muda
atakapojirekebisha na kufikiria ufumbuzi wa kuupata upya tena uhuru wake. Hatua ya kwanza ni: Kubaki mwaminifu kwa wewe mwenyewe!
Hatua ya pili ni: Fanya angalisho kwenye mitego uliyotegewa. Usikubali rushwa; fanya iwezekanavyo kusudi uwe na sifa za utendaji kupitia mafunzo mazuri ukichagua fani mahususi unayoifurahia, ambamo unaweza kupatia mshahara wako, kwani kila mfanya kazi stadi ana bei yake.
Hatimaye: Usiujali ubembelezi unaotangulia shauku na tamaa. Na fikiria matokeo ya baadaye. Utakuwa nani basi? Pengine mtu asiyefahamu tena mwelekeo mzuri…
Amri ya Kumi ya Mungu
«Usitamani mali ya mwenzio»
Amri kumi za Mungu zilizotolewa kupitia
Musa zinatutolea ufahamu wa ndani wa yale yanayotendeka duniani, Dunia ambayo Mungu amewapa watu kusudi wanae binadamu wajipatie chakula humo. Lakini mwanadamu ameitendea nini sayari Dunia? Dunia inakua kitu kimoja kilichogawika kwa sehemu, na ni yule aliyerithi au aliyepata utajiri na mali, anayemiliki eneo kubwa ya ardhi anayoiita mali yake. Mwengine naye humiliki tu sehemu ndogo ya mkate mkubwa huo uliokatwa vipande vipande ambao ni dunia.
Mwengine tena hana hata eneo fulani anayomiliki na anafanya kazi kwa ajili ya kupata mkate wake na kwa kulisha vibaya au vizuri jamaa yake, mke na watoto wake.
Uwanjani mwake, mmiliki mkuu wa ardhi, bepari mkuu, hutumikisha wengine, ambao anawaita wafanya kazi na watumishi wake. Mwenyewe huishi vizuri sana na, kupitia kazi ya mwenziwe, anajinufaisha na vitu vyote vinavyofaa kwa maisha yake ya ubinafsi. Halazimishwi, kama wafanyakazi wake, kupata mkate wake siku baada
ya siku kwa jasho la paji la uso wake. Wengine hujihusiha na hayo kwa manufaa yake.
Watumishi na wafanyakazi wanapokea mshahara wao na mumiliki mkuu wa ardhi yeye hujitengea mtaji anaouzidisha kwa kuwekeza vema ili kukuza mara tena mali yake.
Kukosa usawa huko kunakojitokeza mara na mara huleta wivu, chuki, tamaa na kadhalika, si jambo la mshangao Tukizingatia kusudio la jamii ya siku hizi inayotaka kwamba matajiri watajirike mno na maskini wawe maskini sana.
Hayo yanasisitiza ukweli wa Amri ya kumi ya Mungu. Tayari Yesu wa Nazareti alisema: «Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu». Sentensi hiyo inaweza kutumiwa kuhusu mgawanyiko wa dunia kwa sehemu tofauti. Matajiri wa sasa hujihusisha kwa kiwango kidogo mno na maneno ya Yesu tofauti na hapo kale, ambapo vigezo vya matendo ya kila mmoja vilikuwa maadili ya moyo na matendo yasiotegemea faida kwa mwenziwe. Siku za leo, kila mmoja hajali tena mwenziwe.
Ijapokuwa, yaliyokuwa na thamani jana hata leo yana thamani: hakuna mtu atakayebeba pesa na mali kwenye ulimwengu wa nafsi. Hakuna kilichobadilika, ilikuwa hivyo kwa matajiri wa kale
na ni hivyo pia kwa matajiri wa leo. Hata mmoja miongoni mwao hapiti kwenye tundu la sindano kwa sababu, ufalme wa Mungu bado ni mbali sana na matajiri.
Nafsi zao potovu zitakuwa mahali gani wakati utajiri hautakuwa na umuhimu tena? Kanuni ya panda na vuna itajihusisha na kuleta tena usawa. Ndio sababu kutamani mali ya mwenzio hakuna faida. Hata hivyo, Dunia ni Sayari ya Mungu na siyo kazi ya kujipendelea kwa mwanadamu.
Yule anayeelewa maana ya Amri Kumi za Mungu zilizotolewa kupitia Musa, hutambua ya kwamba, mtu asipotekeleza Neno la Mungu, mtu huyo anakosea, haelewi yeye ni nani, wala hajui kwa nini amezaliwa mara tena duniani.
• Mnaishi milele. Hakuna mauti
• Usikate tamaa! Stahimili!
• Mungu ndani mwetu
• Kumpata Mungu! Wapi? Na Vipi?
• Mafundisho ya Yesu Mlimani







Yesu wa Nazareti alikuwa nani?
Utoto na ujana wake
Kitabuni humu mekusanywa vifungu tofauti vya ufunuo wa Kristo, ambamo mwenyewe anaeleza hadithi ya maisha yake duniani katika Yesu wa Nazareti, kwa upekee ujana na utoto wake.
S170swa • ISBN 978-3-96446-226-8 • Kurasa 46
Jifunze kuomba
Katika sala ya kweli, unapata maarifa ya Mungu.
Sala halisi humfanya mtu awe mwenye raha.
Ila, sala halisi huhitaji mafunzo, kwa kuwa, sala halisi tunayoifanya ndani mwetu wenyewe ni mazungumzo na Mungu.
S174swa • ISBN 978-3-96446-225-1 • Kurasa 54
Vitabu hivi vinapatikana pia katika lugha ya kiingereza, kifaransa na nyingine nyingi pia
Infos at WhatsApp/ Viber in English : + 49 151 1883 8742
Infos par WhatsApp en français : + 49 159 08 45 45 05 www.gabriele-publishing.com