Rasilimali za pamoja: Chachu ya Mabadiliko na Fursa Afrika Muhtasari Stéphanie Leyronas, Benjamin Coriat, and Kako Nubukpo (eds.) Tafsiri: Alliance française de Dar es-Salaam
Kitabu hiki kinaelezea aina nyingi za maendeleo zinazopendekezwa na watu wa Afrika, watumiaji, na wananchi. Mbali na kusimamia mali na rasilimali zinazoonekana na zisizoonekana kwa pamoja, wanajaribu kutumia dhana ya "ushirika" ambayo ilianzishwa kwa kuzingatia maadili kama vile jamii, ushiriki, usawa, na uaminifu. Katika utekelezaji, mbinu yao inachukua mfumo wa ardhi ya pamoja, vyama vya ushirika vya makazi, utamaduni mchanganyiko au maeneo ya