Skip to main content

Swahili Biblical Heliophysics - The Mighty Sun

Page 1

Heliofizikia ya Kibiblia - Jua Lenye Nguvu Ee Bwana, adui zako wote na waangamie vivyo hivyo; bali wampendao wawe kama jua litokalo kwa nguvu zake. Waamuzi 5:31 Kwa maana Bwana Mungu ni jua na ngao; Bwana atatoa neema na utukufu; hatawanyima kitu chema hao waendao kwa unyofu. Zaburi 84:11

Pentateuki Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenganishe mchana na usiku; nayo iwe ishara, na majira, na siku, na miaka; nayo iwe mianga katika anga la mbingu ili iangaze dunia; ikawa hivyo. Mungu akafanya mianga miwili mikubwa; mwanga mkubwa kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku; akafanya na nyota pia. Mungu akaziweka katika anga la mbingu ili iangaze dunia, na kutawala mchana na usiku, na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Na jioni na asubuhi vikawa siku ya nne. Mwanzo 1:14-19 Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu; na tazama, hofu ya giza kuu ikamshika. Ikawa, jua lilipochwa, kukawa na giza, tazama, tanuru ya moshi na taa inayowaka ikapita kati ya vipande hivyo. Mwanzo 15:12,17 Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari. Mwanzo 19:23 Akafika mahali fulani, akakaa huko usiku kucha, kwa sababu jua lilikuwa limetua; akatwaa mawe ya mahali hapo, akayaweka kama mito yake, akalala mahali hapo. Mwanzo 28:11 Na alipopita Penueli jua likamchomozea, akachechemea kwa paja lake. Mwanzo 32:31 Akaota ndoto nyingine tena, akawasimulia ndugu zake, akasema, Tazama, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikanisujudia. Mwanzo 37:9 Wakakusanya kila asubuhi, kila mtu kama ulaji wake ulivyokuwa; na jua lilipowaka moto, kikayeyuka. Kutoka 16:21 Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; wakachukua jiwe, wakaliweka chini yake, naye akaketi juu yake; nao Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande mmoja, na mwingine upande mwingine; mikono yake ikatulia hata jua lilipotua. Kutoka 17:12


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Swahili Biblical Heliophysics - The Mighty Sun by Filipino Tracts and Literature Society Inc. - Issuu