Waraka wa Kwanza wa Yohana SURA YA 1 1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu kulishika, la Neno la uzima; 2 (Kwa maana uzima ule ulidhihirishwa, nasi tumeuona, na twashuhudia na kuwapasha habari ule uzima wa milele, ule uliokuwa kwa Baba, ukadhihirishwa kwetu;) 3 Hilo tuliloliona na kulisikia, tunalihubiri kwenu, ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi; na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. 4 Tunawaandikia ninyi mambo haya ili furaha yenu ikamilike. 5 Basi, hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala hamna giza hata kidogo ndani yake. 6 Tukisema kwamba tuna ushirika naye, lakini tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli. 7 Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. 8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani yetu. 9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. 10 Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo, wala neno lake halimo mwetu. SURA YA 2 1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki. 2 Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu, wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. 3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. 4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. 5 Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika hakika; 6 Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda. 7 Ndugu, siwaandikii amri mpya, bali amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Amri ya zamani ni neno mlilolisikia tangu mwanzo. 8 Tena ninawaandikia amri mpya, ambayo ni kweli ndani yake na ndani yenu, kwa sababu giza linapita na ile nuru ya kweli inang'aa. 9 Yeye asemaye yumo nuruni, naye anamchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa. 10 Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.
11 Lakini anayemchukia ndugu yake yu gizani na anatembea gizani, wala hajui aendako, kwa sababu giza limempofusha macho. 12 Ninawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu kwa ajili ya jina lake. 13 Nawaandikia ninyi akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Ninawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmemjua Baba. 14 Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. 15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita pamoja na tamaa zake, lakini yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. 18 Watoto, ni wakati wa mwisho; kwa hiyo twajua ya kuwa ni mara ya mwisho. 19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu; kwa maana kama wangalikuwa wa kwetu, bila shaka wangalikaa pamoja nasi; 20 Lakini ninyi mmepakwa na Yeye Aliye Mtakatifu, nanyi mnajua mambo yote. 21 Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamuijui iliyo kweli, bali kwa sababu mnaijua, na kwamba hakuna uongo utokao katika kweli. 22 Ni nani aliye mwongo isipokuwa yeye anayekana kwamba Yesu ni Kristo? Yeye ni mpinga-Kristo, anayemkana Baba na Mwana. 23 Kila amkanaye Mwana, huyo hana Baba; (lakini) amkiriye Mwana anaye Baba pia. 24 Basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hayo mliyoyasikia tangu mwanzo yakikaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 25 Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele. 26 Nimewaandikia ninyi mambo haya kuhusu wale wanaowapotosha. 27 lakini upako ambao mmeupokea kwake unakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu ye yote kuwafundisha; ninyi, mtakaa ndani yake. 28 Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake; ili, atakapotokea, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike mbele zake katika kuja kwake. 29 Mkijua ya kuwa yeye ni mwadilifu, mwajua ya kuwa kila mtu atendaye haki amezaliwa na yeye. SURA YA 3 1 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; kwa sababu hiyo ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; maana tutamwona jinsi alivyo. 3 Na kila mtu aliye na tumaini hili ndani yake anajitakasa kama yeye alivyo mtakatifu. 4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi;