Skip to main content

Swahili - Stars in Scriptures (Stellar Astronomy)

Page 1

Nyota katika Maandiko Matakatifu Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota, ulizoziratibisha; Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Na mwanadamu hata umjali? Zaburi 8:3-4

Pentateuki Mungu akafanya mianga miwili mikubwa; mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. Mwanzo 1:16 Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, uzihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Mwanzo 15:5 Kwamba katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zake; Mwanzo 22:17 Nami nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; Mwanzo 26:4 Akaota ndoto nyingine tena, akawasimulia ndugu zake, akasema, Tazama, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikanisujudia. Mwanzo 37:9 Mkumbuke Ibrahimu, Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha uzao wenu kama nyota za mbinguni, na nchi hii yote niliyoinena nitawapa uzao wenu, nao watairithi milele. Kutoka 32:13 Nitamwona, lakini si sasa; Nitamtazama, lakini si karibu; Nyota itatoka kwa Yakobo, Na fimbo ya enzi itainuka kutoka Israeli, Nayo itazipiga pembe za Moabu, Na kuwaangamiza wana wote wa Shethi. Hesabu 24:17 BWANA, Mungu wenu, amewazidisha, nanyi, angalieni, leo mmekuwa kama nyota za mbinguni kwa wingi. Kumbukumbu la Torati 1:10 Na usije ukainua macho yako kuelekea mbinguni, na utakapoona jua, na mwezi, na nyota, jeshi lote la mbinguni, ukalazimishwa kuviabudu na kuvitumikia, ambavyo BWANA, Mungu wako, amevigawanya kwa mataifa yote chini ya mbingu zote. Kumbukumbu la Torati 4:19


Turn static files into dynamic content formats.

Create a flipbook
Swahili - Stars in Scriptures (Stellar Astronomy) by Filipino Tracts and Literature Society Inc. - Issuu