Sheria za Kibiblia za Nguvu Nguvu kamili ya Yesu Kristo haiharibiki.
Yesu akaja, akasema nao, akisema, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafundishe mataifa yote, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; mkiwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Amina. Mathayo 28:18-20 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa dunia. Matendo 1:8
Pentateuki Nanyi mnajua ya kwamba nimemtumikia baba yenu kwa nguvu zangu zote. Nina uwezo mkononi mwangu kukudhuru; lakini Mungu wa baba yako aliniambia jana usiku, akisema, Jihadhari, usimwambie Yakobo neno jema wala baya. Mwanzo 31: 6,29 Akasema, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli; maana umeshindana na Mungu na wanadamu, nawe umeshinda. Mwanzo 32:28 Reubeni, wewe u mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, na mwanzo wa nguvu zangu, ubora wa heshima, na ubora wa nguvu. Mwanzo 49:3 Nami kwa kweli nimekusimamisha kwa sababu hii, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, na jina langu litangazwe katika dunia yote. Kutoka 9:16 Mkono wako wa kuume, Ee Bwana, umetukuka kwa nguvu; Mkono wako wa kuume, Ee Bwana, umewavunja-vunja adui. Kutoka 15:6 Ikiwa bwana wake hakumpendeza, aliyemposa, ndipo atamwacha akombolewe; hatakuwa na mamlaka ya kumuuza kwa taifa la kigeni, kwa kuwa amemtendea kwa hila. Kutoka 21:8 Musa akamsihi Bwana, Mungu wake, akasema, Bwana, kwa nini hasira zako zinawaka juu ya watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri kwa uweza mkuu na kwa mkono wenye nguvu? Kutoka 32:11 Nami nitavunja kiburi cha nguvu zenu; nami nitazifanya mbingu zenu kuwa kama chuma, na nchi yenu kuwa kama shaba; Nao wataanguka mmoja juu ya mwingine, kama vile mbele ya upanga, asipofukuzwa na mtu; wala hamtakuwa na uwezo wa kusimama mbele ya adui zenu. Mambo ya Walawi 26 :19,37 Na sasa, nakuomba, nguvu za Bwana wangu na ziwe kuu, kama ulivyosema, ukisema, Hesabu 14:17 Balaamu akamwambia Balaki, Tazama, nimekuja kwako; je, nina uwezo wowote wa kusema neno lo lote? Neno ambalo Mungu atalitia kinywani mwangu ndilo nitakalolinena. Hesabu 22:38