Ukweli Kamilifu wa Kibiblia Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Yohana 14:6 Jitahidini kweli hata kufa, naye Bwana atawapigania. Mhubiri 4:28
Pentateuki Akasema, Na atukuzwe Bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, ambaye hakumsahau bwana wangu rehema zake na uaminifu wake; mimi nilipokuwa njiani, Bwana aliniongoza hata nyumba ya nduguze bwana wangu. Mwanzo 24:27 Sistahili hata kidogo rehema zote na uaminifu wote uliomtendea mtumishi wako; maana nilivuka mto huu wa Yordani kwa fimbo yangu; na sasa nimekuwa makundi mawili. Mwanzo 32:10 Mpelekeni mmoja wenu, akamlete ndugu yenu, nanyi mtafungwa gerezani, ili maneno yenu yathibitishwe, kama mna kweli yo yote; la sivyo, aishivyo Farao, ninyi ni wapelelezi. Mwanzo 42:16 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu wote watu wenye uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wanaochukia tamaa; ukawaweke juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mamia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa makumi; Kutoka 18:21 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma na neema, mvumilivu, mwingi wa rehema na kweli, Kutoka 34:6 Ndipo utakapouliza, na kuuliza kwa bidii; na tazama, ikiwa ni kweli, na jambo hilo hakika, ya kuwa chukizo kama hilo limefanyika kati yako; Kumbukumbu la Torati 13:14 Yeye ndiye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; maana njia zake zote ni hukumu; Mungu wa kweli, asiye na uovu; Yeye ndiye mwenye haki na adili. Kumbukumbu la Torati 32:4
Historia Basi sasa mcheni BWANA, mkamtumikie kwa unyofu wa moyo na kweli; na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri; mkamtumikie BWANA. Yoshua 24:14 Mchongoma ukaiambia miti, Mkinitia mafuta kweli niwe mfalme juu yenu, basi njooni mkae kivulini mwangu; na kama sivyo, moto na utoke katika mchongoma na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni. Waamuzi 9:15 Mcheni BWANA tu, mkamtumikie kwa uaminifu kwa mioyo yenu yote; maana angalieni mambo makuu aliyowatendea. 1 Samweli 12:24