Sehemu za kitabu
MUNGU anaponya
cha Gabriele
Madondoo toka kitabu cha Gabriele, nabii na mjumbe wa Mungu :
MUNGU anaponya Nguvu kubwa mno isiyokadiriwa na kuwaziwa inatenda kazi ndani ya kila mmoja wetu. Ni nguvu ya upendo, nguvu ya Mungu. Gabriele anatoa maelezo kitabuni humu kwamba afya na uponyaji vinategemea mpango wa msingi wa utu wetu wa ndani na kwamba hisia na fikra zetu vina ushawishi mkubwa juu ya hali yetu njema ambayo tunaweza kuamsha ndani mwetu kwa kumgeukia Mungu, chemchem ya nguvu ndani mwetu. Kwa kutumia maneno yenye kugusa moyo na inayojaa ujuzi, kitabu hiki kinatuelekeza jinsi ya kuamsha nguvu za kimungu ndani mwetu ili kutia nguvu nafsi na mwili wetu. Hayo haimzuii kamwe mtu kumwendea daktari wake. S 309TBSW • ISBN 978-3-96446-377-7 • Kurasa 112
1st Edition in Swahili: October 2024 1ère édition en Swahili: Octobre 2024
No. Ref./ N° Réf.: G362sw The German edition is the work of reference for all questions regarding the meaning of the contents Pour toute question se rapportant au sens, l'édition allemande fait référence © All Rights Reserved / Tous droits réservés Gabriele-Verlag Das Wort GmbH
Sehemu za kitabu
MUNGU anaponya
Je! Moyoni mwa mwanadamu hamna matumaini na tamaa chungu nzima kutokana na neno uponyaji! Uponyaji huleta nafuu, faraja na ukombozi, uponyaji huleta amani mahali panapo kasoro. Neno «uponyaji» linamaanisha mchakato unaoongoza kwenye afya na sio hatima ya mchakato huu ambayo ni tendo la mtu kupona. Ni nani asiyehitaji uponyaji? Ni nani asiyelalamika kuhusu tatizo kubwa zaidi la kiafya ambalo angelitamani likome? Mtu aliye bado na moyo mkunjufu huta mbua kwamba uponyaji, mchakato wa uponyaji na kuponywa, vinahusiana na mpangilio asilia wa utu wa ndani. Uponyaji, kwa mjibu wa maana yake ya kina kabisa, hugusa nyanja za nafsi zinazounda asili ya mwanadamu na ambamo mna uzima wake halisi.
1
Twawezaje kuwasiliana na chemchemi ya nguvu za uponyaji?
N guvu kuu mno ndani ya mwanadamu ni Roho. Mungu ndiye nguvu ya msingi ya kila kiumbe. Roho huyo wa kimungu wa ulimwenguni pote ni uzima ndani ya aina zote za viumbe, hata pia ndani ya aina zote za viumbe vyenye maada. Pumzi yake iliyo uzima hutia uhai nafsi na kila seli ya mwili wa mwanadamu. Kwa hiyo Roho ni uhai, nguvu ya uzima, nguvu inayotibu. Ikiwa tunataka kupata uponyaji kupitia Roho, ni lazima tuupe uhai kila kitu kinachohusiana na mchakato wa uponyaji, yaani, kujaza uhai mawazo na maneno yetu. (...) Mwanadamu anaweza kuepuka magonjwa, wasiwasi na bahati mbaya ikiwa atafahamu asili yake, ambayo ni Roho, na kutamani maendeleo makubwa ya kiroho kwa kujitahidi kutambua sheria za kiroho za kimungu. Amri kuu, iliyo muhtasari wa amri zote ni upendo. (...)
2
Zama ya atomu. Zama ya Mabadiliko ya hewa. Mtiririko wa nguvu za ulimwenguni kote. Dunia inayumbayumba. Ni mahali ipi pa kupata msaada hakika?
U tu wetu asilia wa milele ni wa mwana wa yule asiye na mwisho, mwana wa Baba wa milele. Hatuna chaguo lingine isipokuwa kugeukia upande wa nguvu hiyo ya ulimwenguni kote, upande wa Mungu, kwa sababu sisi ni wana wa ulimwenguni kote na warithi wa umilele. (...) Roho wa milele anayeleta wokovu na uzima, yaani Mungu, upendo, hawaachilii wanadamu. Jinsi dhiki ya mwanadamu inavyokua, ndivyo Roho anavyotenda kazi kwa bidii katika uli mwengu huu. Anawafundisha wanae na ana wapa unafuu na uponyaji. Hata hivyo, ni lazima waweze kuthibitisha na kutambua Roho, uzima, Mungu ndani mwao, kama chanzo cha nguvu. Hii ni hatua ya kwanza kuelekea uponyaji wa kiroho. (...) 3
Hakuna kinachopotea. Tunavuna tulichokipanda
H akuna kinachopotea. Apandacho mwa nadamu ndicho atakachokivuna isipokuwa tu akijitahidi kujichunguza na kutambua mambo mabaya ya ndani mwake. Baadaye anaweza kufahamu upesi sana tabia zake potovu, kutambua ukiukaji wake wa sheria ya Mungu na mara moja kujitahidi kuyarekebisha. Tuseme basi kwamba hayo ni maisha ya kiroho yenye dhamiri safi. Ajuaye kwamba kila kitu ni nguvu na kwamba hakuna nguvu inayopotea, pia anajua kwamba kila jambo tunalolitoa linaturudilia: nguvu, hisia, mawazo, maneno, matendo, tendo nzuri au mbaya, hofu, chuki, wivu, uadui na wivu. Fikra, matendo, maneno na hisia zetu vinaingia nafsini mwetu ndivyo vinaunda mwonekano wa nje wa mwili wetu. (...)
4
Uamsho wa nguvu za kiroho. Sala sahihi. Ukimya
M wanadamu yumo ndani ya shule ya maisha. Kwake, Dunia ni mahali pa majifunzo ambapo anaweza kubadilika. Ni lazima tutambue fursa hiyo na kujitahidi kutakasa roho zetu zilizo urithi wetu wa ulimwenguni kote, kwa kujitoa, tayari kama wanadamu, kwa lengo halisi la maisha, huku tukiamsha ndani mwetu nguvu za kiroho, nguvu za Mungu, ambazo pia zinaponya, ili zitiririke kwa wingi zaidi ndani mwetu. Ni lazima tufanye bidii kwa kurekebisha hali zetu mbovu ili tuweze kuzaliwa upya katika Roho, kupata wokovu wa ndani na hivyo kupata uponyaji utokao kwa Roho. Ni lazima tuheshimu sheria ya uzima. Kwa njia hiyo tutaizibua ndani mwetu chemchemi inayotaka kunywesha kila seli ya mwili wetu. (...)
5
Fikra nzuri au chanya huipandisha roho na mwili kwenye uwanja wa juu wa mtetemo. Kudhibiti vema fikra zako ni kuongoza vema maisha yako
H ayo yana maana kwamba kufikiri vema
ni kuishi vema. Mtu asiyechunguza mawazo na asiyejidhibiti mwenyewe pia anapotoka kutokana na nguvu za ushawishi za mazingira ambamo anaishi, kwa maana mawazo na maoni hutokana na ushawishi wa mazingira iliyoundwa na watu wenzetu. (...) Hali hiyo haiwezi kujitokeza yenyewe. Ni lazima tufanye juhudi na kuongoza vema maisha yetu. Tunapaswa kuibadilisha ili ipate hekima na nguvu. Kwa kufanya hivyo, lazima uishi kwa uangalifu! Nguvu chanya basi itabadilisha nguvu hasi au mbovu zinazotushikilia bila ya sisi, mara nyingi, kuzitambua. Hivyo basi tutajazwa na kuishi kikamilifu, kwa uangalifu, kila siku, kila saa na kila dakika, hali hiyo itatufanya kuwa wenye raha kwa sababu kwa kufanya hivyo tunapata nguvu nzuri. Nguvu hizi huboresha maisha yetu na tunazidi kutimiza mapenzi ya Mungu. 6
Mawazo yetu mazuri hufungua chemchemi ya nguvu ndani mwetu
Yote yaliyo mema, safi, adhimu, nguvu zote chanya, hutoka ndani sana ya nafsi yetu, yanatokea kwenye kiini cha msingi kisichobadilika, yanatokea kwa Mungu. Tukifuata sheria ya Mungu, na tukiwa na uhusiano mwema na nguvu zote, siyo tu kwamba tutahifadhi nguvu yetu ya ubunifu lakini tena nguvu hiyo itaendelea kuongezeka. Lakini tukikata mawasiliano na Mungu, kwa kufikiria na kutenda kwa hali ya kiutu sana, kwa hali ya uovu, tukipanda chuki, kijicho na mafarakano, tukichochea fikra za wivu, tutapoteza nguvu kiroho na kimwili. Kifaa cha umeme hufanya kazi tu kikiwa kimeunganishwa na mkondo wa umeme. Ila Ikiwa umeme umekatwa, kifaa hakifanyi kazi tena. Ni mamoja pia kwa wanadamu. Tukitenda kinyume na sheria ya ulimwengu kote, dhidi ya nguvu za maisha, kwa kutoweka kwa dhati maisha yetu mikononi mwa Roho na kwa kuishi maisha isiyo na nidhamu, nguvu za kiroho hupunguka nafsini na mwilini. Jinsi nguvu 7
zinavyopunguka, ndivyo viungo hudhoofika na hivyo huwa tayari kupatwa na maradhi. Uzaifu utatukumba, mtetemo wetu utapunguka. (...) Ikiwa tunataka kupata afya na kuchochea mwili wetu kupona kupitia nguvu za Roho, ni lazima tufuate sheria hizo za Uzima: Nguvu mbaya, zilizoharibika zina uwezo wa kusumbua nafsi na mwili. Kinyume chake, nguvu nzuri, safi, za kimungu huimarisha mwili na nafsi, na hivyo huleta afya. Uponyaji basi unaweza kutokea ndani na kwenda nje, kupitia nguvu za Mungu ndani mwetu. Kwa hiyo ni lazima kwanza tujitoe kwa nguvu chanya, kwa kuzishinda nguvu zetu hasi ambazo ni hisia, mawazo, maneno na matendo mabaya, kwa kuvipinga na mawazo, maneno na matendo chanya, ya uthibitisho, yenye kujenga. Baadaye, tutaweza kukaribisha ndani mwetu nguvu chanya ambayo pia ni nguvu ya uponyaji na ya uzima. Hivyo, kabla ya kuamsha nguvu za ndani, ni lazima tujikomboe toka fikra mbovu, kufuta akilini wazo lote linalotukumbusha ugonjwa, la sivyo, mawazo hayo yanaweza kusababisha maradhi mengine au kudumisha ugonjwa mwilini. (...) 8
Fikra ni nguvu. Jinsi tutakavyoendelea kuwa na wazo fulani, ndivyo itakavyokuwa kubwa na kutulemea. Hata kama jambo hili si rahisi, wakati tunapoteswa, tungelipaswa kutambua kwamba kwa msaada wa fikra chanya, tunaweza kushinda maovu mengi ndani mwetu au kujiandaa kupokea nguvu chanya. Tuwe na ujasiri wa kuchukua kwamba maumivu, ugonjwa, magumu na shida zetu hutokana na baadhi ya sheria! Tujaribu kuwa na matumaini kwa uwezo na nguvu ya Roho anayeweza yote. Tutaweza kupata basi maarifa kwamba nguvu ya Mungu ipo, inaleta nafuu, inaponya, inatusaidia na kutuongoza. (...)
9
Kristo, tabibu wa ndani na mponyaji wa nafsi zetu
N guvu ya kiroho, na ya uponyaji, tunayoi-
hitaji hapa ni nguvu ya Kristo inayofanya kazi ndani mwetu. Kristo ndiye tabibu na mponyaji wa ndani. Nguvu Yake ina uwezo wa kuingia mwilini mwetu na kuondoa maovu yanayotuathiri. Hata hivyo, nguvu hiyo inaweza tu kutenda kazi ikiwa tunaweka mawazo yetu ya uponyaji ndani Mwake na kuyajaza na upendo wa kina kwa Yeye aliye mbali na magonjwa yote na shida na anayejua afya tu. Tungepaswa kufuta kwenye mawazo na maneno yetu msamiati unaohusiana na ugonjwa, kama vile «kuwa mgonjwa», ili mawimbi ya uponyaji wa kiroho yaweze kutimiza matakwa yetu ya uponyaji. Yanainua nafsi na mwili wetu kwa mtetemo wa juu ambao unaruhusu uponyaji wa nafsi yetu kwa tendo la daktari na mponyaji wa kiroho. Na kwa sababu hayo ni muhimu kwa nafsi, mwili wetu pia unapata uponyaji kupitia nafsi. Kristo, tabibu wa ndani na mponyaji ambaye tunamtolea ombi letu, 10
huponya nafsi kabla ya yote. Iwapo nafsi ina afya bora, basi inawasilisha nguvu nzuri za uponyaji kwa mwili wetu. (...)
Kubadili mivutano, kuchangayikiwa, hasira na utulivu au ukimya
N i katika ukimya ndipo nguvu hutenda
kazi, ndipo uponyaji wa roho na mwili wetu unakamilishwa. Hii ndiyo sababu lazima kwanza tufikie ukimya wa ndani, ili mawimbi ya uponyaji wa kiroho yaweze kufanya kazi. Ikiwa ni vigumu kwetu kupata utulivu huo wa ndani, tusikasirike wala kung'angania kuupata, bali tujithahidi kuwa watulivu na kusitawisha fikra zenye kutuliza. Mwili wetu huwa unajibu hapo hapo kwa aina ya mwendo wa mwili na mawazo yanayotutawala. (...)
Tunaweza kuchukua jumla ya hisia zetu kama uso wa ziwa la maji lililopigwa na dhoruba kali. Kisha kwa ghafla, upepo ukitulia, na mawimbi yakitoweka ziwa hurudi kuwa tulivu na laini kama kioo. Kufikiria mfano huo 11
wa ziwa pia ni njia ya kutuliza ulimwengu wa hisia zetu. Mivutano na misukosuko ya ndani mwetu yanaweza basi kutoweka. Tungepaswa kuipa kipaumbele maalum dhamiri ya mfumo wetu wa neva. Mti huu wa uzima ulio ndani ya mwanadamu una jukumu kubwa mwilini mwetu, na unachangia kwenye afya au magonjwa. Sababu kadhaa zinaweza kuwa chanzo cha kuchanganyikiwa kwetu. Wasiwasi inaweza kutokana na mkazo wa sasa wa mishipa yetu au sababu ya zamani ambayo inaweza pia kuwa ya asili ya uovu tuliotenda katika maisha ya awali duniani. Tofauti na hisia na mawazo yetu ya uponyaji, ikiwa mfumo wetu wa neva una shida au umefadhaika, nguvu ya Kristo haiwezi kutiririka vema humo. Nguvu ya Kristo inaweza tu kutiririka ndani ya mwili ikiwa dhamiri ya mfumo wetu wa neva, ambamo unapitia, inatulia. Hivyo, mkazo wowote unadhuru, iwe kama unasababishwa na namna mbovu ya kufikiri au kutokana na wasiwasi. Ikiwa mfumo wetu wa neva hauna amani, nguvu ya milele, ya amani na inayoleta utulivu haiwezi kutupa msaada, nafuu na uponyaji – jinsi Mungu angetaka iwe hivyo. Ikiwa unataka kurejelea nguvu za Roho 12
na kuzipa nafasi ya kwanza maishani mwako, ni muhimu kujua kwamba hayo hayafanyiki siku moja baada ya nyingine. Iwe nafsi wala mwanadamu hawezi kwa muda mfupi kuachana na dhana na mazoea yao ya zamani ambayo sasa yana mizizi mirefu.
Kila mtu lazima atambue wajibu wake. Mabadiliko huanza na mtu binafsi
Ikiwa tunataka kuishi katika afya bora, ni
lazima tumwone na kumhisi Mungu ndani ya vitu vyote, kutimiza amri za ulimwenguni pote, za upendo usio lenga faida, za amani na za maelewano. Kuona yaliyo safi, bora,mema na makuu katika aina zote za viumbe na kuwa na heshima kwa kila kiumbe bila kuridhika tu na kuongea kuhusu maisha, Mungu na kuhusu yote ambayo yanapaswa kufanywa ili kufikia ulimwengu bora. Kila mtu anaombwa kujichunguza mwenyewe. Anayejifunza kubadilika, kufikiri na kuishi kulingana na Amri za Mungu, anainua mwanga wake mwenyewe. Anatoa maisha yake kwa 13
Mungu. Hana tena mawazo mabaya, mawazo ya uharibifu na hivyo basi hadumishe tena hali mbaya hizo. Tofauti na hayo, anaishi kwa amani na jirani yake, na Dunia na viumbe vyote. Amani hutokana tu na mtu mwenyewe, na kila mtu peke yake, ikiwa anajitahidi kufikiria na kuishi bila kutegemea faida na kwa heshima ya uzima. Kila mtu hutenda kazi kwa dhati sio tu kwa manufaa ya maisha yake mwenyewe na ya wanadamu wenzake, lakini pia kwa manufaa ya Ardhi na viumbe vyote viishimo. Kwa hiyo kila mtu ni muwajibikaji wa nafsi yake mwenyewe, mawazo na matendo yake. (...) Kwa hiyo, hatupaswi kufikiria kwamba ni jirani yetu, kanisa au Serikali ndiyo inapaswa kubadilika. Kila mmoja wetu ameombwa kubadilika. Hiyo ndiyo njia pekee ya kufanikiwa katika kutoa nguvu chanya, zenye kujenga na hivyo kutenda mema – kuungana na wengine wengi wanaokuwa na msimamo huo – kwa wale ambao wangali bado katika kivuli cha tamaa ya mali. Kwa njia hiyo sisi pia tunatenda vyema duniani ambayo sisi ni sehemu yake. 14
Yesu alisema: «Mnachowafanyia walio wa dogo kati ndugu zangu, mnanitendea Mimi.» Mungu ni yote katika mambo yote. Kile tunacho mtendea jirani yetu, na viumbe vyote, kitatuathiri wenyewe. Ikiwa tunataka kuinua mtetemo wa nafsi yetu na mwili wetu, lazima tubadili mwenendo wetu. Basi, kwa msaada wa nguvu ya Kristo, utu wetu, mtetemo wetu, utasafishwa na kuinuka ikiwa hisia zetu, mawazo, maneno na matendo yetu ni chanya na kwamba tunaanza kuishi maisha yasiyolenga faida, kumheshimu jirani yetu, kumpenda, kumtendea mema, kuthamini uzima wa Ardhi na wa viumbe. (...)
15
Sisi ni watoto wa Mungu. Chemchemi ya nguvu na afya inapatikana ndani mwetu. Inabidi tufute akilini mwetu mawazo mabaya
N i vema taswira ya magonjwa, matatizo,
hofu, wasiwasi na dhiki ifutike kwenye fikra zetu. Ni lazima jitihada zetu zote ziwe za kutochukua tena hali za kibinadamu kama vile ugonjwa, kama hali ambayo ni lazima tuponywe nayo. Katika fikra, na kwa imani ya kina, ni vema tuchukue kwamba magonjwa na maovu mengine yote hayapo! Badala ya kufikiria sana kuhusu ugonjwa, wasiwasi, shida na matatizo mengine, tuthibitishe afya, furaha, amani, ridhaa na raha! Tunapaswa kuchukua muda wa kutafakari kuhusu nguvu takatifu ya Mungu, mng'ao wake safi, uhalisia uliofichwa nyuma ya kivuli cha ugonjwa, mateso, dhiki na wasiwasi – hayo bila kujali hali ya nje, kwa mfano, hatari ya ugonjwa au maambukizi. Hivyo matokeo yake ni kwamba, tunainua mtetemo wetu, nuru yetu inang'aa vema na dalili za ugonjwa zinabadi lika. Kila mmoja wetu, kupitia utu wake halisi, 16
ni mwana wa Aliye Juu Zaidi na ana ndani mwake uzima wa kimungu. Kulingana na asili yetu, sisi ni wa Mungu. Ukamilifu unaoambatana na utu wetu halisi ni afya, amani na raha. Hebu tuyatafakari maneno haya: sisi ni wana wa Mungu, tunamiliki ujazo wote usio na mwisho, afya, amani na raha. Tungepaswa basi kumgeukia Mungu, nguvu na ujazo wa milele, sio kuzungumza kuhusu magonjwa yetu na upungufu wa mali. (...) Lazima chuki iondoke maishani mwetu. Inatupasa kumchukua jirani yetu kama rafiki na ndugu. Tunapata amani ya roho katika kudhibiti hisia mbaya zetu zote. Ni kupitia amani hiyo ndiyo nafsi na mtu wanapata uponyaji. Kama vile vitu vyenye maada vinaheshimu kanuni ya magnetisi, mawazo yanafuata kanuni ya mvuto. Kwa hiyo, tutambue kwamba ugonjwa si kitu kingine bali ni ubainifu wa mawazo yetu! Kile tunachovuta kupitia fikra huchukua nafasi ndani mwetu, kwani ndani mwetu tuna mambo iliyo sawaswa na hayo au yanayoyafanana. Vitu vinavyofanana hujikusanya pamoja. 17
Tunapaswa kubadili namna yetu ya kufikiri. Uthibitisho wa asili yetu halisi unasababisha uponyaji. Uponyaji wa kiroho ni mchakato ambapo mwanadamu hujiweka huru toka uovu ambao alisababisha yeye mwenyewe
Tungepaswa kutambua maana ya hayo na kujipanga kulingana na ukweli ufuatao: Mungu, Bwana wetu, hakuumba ugonjwa hata moja. Kwa hiyo, katika uhalisia Wake hakuna magonjwa pia. Kwa hiyo hatupaswi kamwe kufikiri kwamba sisi ni wagonjwa. Hebu tuache hisia zote za ugonjwa na katika mawazo tuthibitishe afya ndani mwetu. Hivyo, dhamiri ya seli zetu itaamka na kutupa nguvu na amani kwa wingi. (...) Tunapaswa kuepusha mawazo yetu na mambo mabaya yanayotukabili kiroho kama vile kimwili, na kujitahidi kuwa na mawazo yenye matumaini na ya kujenga ambayo yanakuza afya. Tukuze mawazo ya afya! Tukitambua na kukubali kwamba Mungu ndiye uzima wetu, tunaelewa kwamba hakuna kitu kinachoweza kuwepo nje ya Mungu. Hebu 18
tumuache ajitukuze ndani mwetu kwa kuthibitisha umungu! Jumla ya mawazo hasi yatatoweka. Ndani mwetu kila kitu kitakuwa wazi, salama na furaha. Ugonjwa ni ubaya. Mungu hakuumba mabaya. Kwa hiyo maovu hayapo. Hata kama maovu yapo katika mazingira ya nje, ya kimaada, katika uzima wetu halisi, ila katika Mungu, hayana uwepo halisi. (...)
19
Sala ya kweli ina utekelezaji ndani mwake
M aombi ni alama ya uhusiano na Mungu. Ila fikra zetu za sala huwa na nguvu sana ikiwa sisi wenyewe tunatimiza ujumbe uliyomo ndani ya sala yetu kila siku. Kwa hivyo nikiomba kwa ajili ya afya, lazima pia nijitahidi maishani kuwa na mawazo ya afya bali sio ya ugonjwa. Hivyo ninajifungua tayari kwa mawimbi ya uponyaji. Ninapoomba kwa ajili ya amani na maelewano na jirani wangu, ingelikuwa heri kuthibitisha sifa zake nzuri, na kutozungumzia vibaya juu yake. (...) Kile ninachokitoa hurejea kwangu! Ikiwa ninamtakia jirani yangu amani na maelewano, na ninaona ndani mwake nuru ya kimungu, basi wema, amani na maelewano hunirudilia. Ninageuka kile ninachoweka katika sala yangu. Ikiwa nataka kupendwa, lazima nijitahidi kumpenda jirani yangu. Ninatoa kulingana na jinsi nilivyo na mwangwi unaorudi kwangu unalingana na kile nili20
chokitoa. Kwa hiyo ni muhimu kubadili mwelekeo wa fikra zetu. Kuomba vema kunaambatana na mwenendo bora maishani. Sala sahihi yanaambatana na utimilifu wa uzima wetu na ni tendo la msingi sana. Kwa hiyo kuomba vema kunamaanisha kuishi vema. Kuomba kwa kweli kunamaanisha kutimiza amri za Mungu, kusamehe jirani, kumpenda na kuelekeza upande wake mawazo mazuri, mema na ya upendo hata kwa adui yetu mwenye uhasama mkali zaidi. Hayo ndiyo sala hai, inayotenda kazi ndani mwetu na kufungua dhamiri yetu kwa mawimbi ya uponyaji wa Kristo. Mtu anayeweza kuomba hivyo kwa moyo wake wote na anayeomba nguvu na msaada wa Mungu ataupokea. (...)
21
Mungu peke yake ndiye anayejua jambo lililo jema kwa wokovu wa nafsi yetu. Mbegu njema peke yake ndizo hutoa mavuno mazuri. Upendo ndio uwezo mkuu na ndio utu wetu halisi
Apandaye upendo atavuna upendo. Ni kanuni ya Roho: kile tunachotoa, tutakipokea. Ila, upendo sio tu kunong'ona maneno matamu kwa kusikia. Upendo pia ni uadilifu na unyofu, ambao ikiwa ni muhimu, huonyesha vipengele vya sheria ya kimungu. Upendo ni kusema mambo ambayo yanahitajika kusemwa. Upendo ni wakati hisia, mawazo na maneno yangu hayana ubinafsi. Upendo ni hayo yote. Tunachokitoa kinaturudilia mara tena, kinachukua mizizi na kutuathiri. Kwa hivyo, kupokea nguvu za uponyaji kunahitaji kuishi maisha ya uadilifu na kutokuwa na ubinafsi. Upendo ni nguvu kuu katika ulimwengu wote. Upendo ndio utu wetu halisi. 22
Kila mmoja wetu kwa mara nyingine tena afikie nguvu hiyo kuu, ya ulimwengu, upendo, ili tuweze kuchangia ustawi na maendeleo ya jamii ya wanadamu na ya kila nafsi kwa kipekee. Hiyo ndiyo ninayowatakia wanadamu wenzangu kwa moyo wote. Gabriele
23
Roho huru – Mungu ndani mwetu Kitabu hiki kinamwelekeza msomaji kwenye njia ya uhuru na kinamuwezesha kujitenga na imani potovu, mila ngumu na taasisi zinazotushikilia. Njia hiyo ni njia iongozayo kwa Mungu, kwa Mungu ndani mwetu. S179SW • ISBN 978-3-96446-247-3 • Kurasa 76
Yesu wa Nazareti alikuwa nani? Utoto na ujana wake Kitabuni humu mmekusanywa vifungu tofauti vya ufunuo wa Kristo, ambamo mwenyewe anaeleza hadithi ya maisha yake duniani katika Yesu wa Nazareti, kwa upekee ujana na utoto wake. S170SW • ISBN 978-3-96446-226-8 • Kurasa 46
Jifunze kuomba Katika sala ya kweli, unapata maarifa ya Mungu. Sala halisi humfanya mtu awe mwenye raha. Ila, sala halisi inahitaji mafunzo. Kwa kuwa sala halisi tunayoifanya ndani mwetu wenyewe ni mazungumzo na Mungu. S174SW • ISBN 978-3-96446-225-1 • Kurasa 54
Maisha niliyochagua mimi mwenyewe Kitabu kinachotoa majibu ya kina kwa maswali mengi: Maisha ni nini kwa kweli? Kwa nini kila mtu ana maisha isiyo na kifani? Je, kwa kweli, bahati ipo? Sababu gani nilizaliwa katika familia hii bali si katika nyingine yote ile? Je ninakabiliwa na majaliwa yangu? Ni nani aliyepangilia tangu awali matukio ya maisha yangu? S 345SW • ISBN 978-3-96446-410-1 • Kurasa 54
24
Amri Kumi za MUNGU na Mafundisho ya Yesu wa Nazareti Mlimani Gundueni Amri Kumi za Mungu zilizofafanuliwa katika usemi wa siku hizi na pia maelezo kuhusu Mafundisho ya Yesu Mlimani iliyofunuliwa na Kristo mwenyewe kupitia Gabriele, nabii na mjumbe wa Ufalme wa milele. Ni maadili ya ulimwenguni pote isiyotegemea dini na inayomlenga kila mmoja aidhuru utamaduni wake. Jaribu mwenyewe, ikiwa inawezekana, kubadili maisha yako. S182TBSW • ISBN 978-3-96446-289-3 • Kurasa 228
Vijitabu vitolewavyo bila malipo • Kumpata Mungu! Wapi? Na Vipi? • Maneno ya faraja • Usikate tamaa! Stahimili! • Mungu ndani mwetu • Hauko peke yako • Mafundisho ya Yesu Mlimani • Mnaishi milele. Hakuna mauti • Yesu na wanyama • Maisha ya raha hadi uzeeni • Hili ni Neno Langu A na Ω • Uwezekano wa kuzaliwa upya katika mwili wa mwanadamu ni neema ya Uzima Vitabu vingine vinapatikana katika lugha ya Kiswahili, kiingereza, kifaransa na nyingine nyingi tena Infos at WhatsApp/Viber in English: + 49 151 1883 8742 Infos par WhatsApp en français: + 49 159 08 45 45 05 www.gabriele-publishing.com
un
gu -
Uzim a
us
io
n
a
ew a
M
ile le
i sh o
Ufalm
mw
o l
um
L ang
bi
en
M
ye
a
n
g
u
li
po
wa z
i - N ji a ie n
da
yo
kw
Gabriele Publishing The Word Max-Braun-Straße 2 • 97828 Marktheidenfed • Germany www.gabriele-publishing.com